Mshambuliaji wa Simba Simon Sserunkuma Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Simon Sserunkuma, amesema kuwa kwasasa hana furaha ndani ya klabu ya simba kutokana na kukosa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Goran Kopunovic. Nyota huyo alisajiliwa wakati wa msimu wa dirisha dogo msimu akitokea kwenye klabu ya Express ya Uganda, kipindi hiki amekuwa na wakati mgumu kutokana na kuwekwa katika risiti ya wachezaji wa akiba kwenye michezo mingi. Akizungumza na mwandishi wetu mchezaji huyo amesema kwasasa anatamani kuondoka klabuni hapo ili akatafute sehemu ambapo ataendelea kuimarisha kiwango chake.