Wachezaji na viongozi wa klabu zilizohusika kupanga matokeo nchini Nigeria kwenye mechi zilizzomalizika kwa ushindi wa 79-0 na 67-0 wamepigwa kifungo cha maisha kujihusisha na mchezo wa soka.
Plateau United Feeders walipata ushindi wa mabao 79-0 dhidi ya Akurba FC wakati Police Machine FC waliichapa Bubayaro FC 67-0.
Vilabu hivyo vinne pia vimefungiwa kujihusisha na mchezo wa soka kwa miaka 10.
Kamati ya shirikisho la soka la Nigeria NFF imependekeza waamuzi wa michezo hiyo miwili nao kupigwa adhabu ya kufungiwa maisha.
Plateau United Feeders na Police Machine waliingia kwenye michezo hiyo wakiwa wanalingana pointi na kilichokuwa kikitazamwa ni tofauti ya mabao ili kuweza kupanda daraja.
Feeders mabao yao 72 waliyafunga kipindi cha pili wakati Police Machine mabao yao 61 waliyafunga kipindi cha pili.
Baadhi ya vipigo vikubwa kwenye soka:
1885: Arbroath 36-0 Bon Accord (Scotland)
1995: Man Utd 9-0 Ipswich Town (Premier League record)
2001: Australia 31-0 American Samoa (World Cup qualifier)
2002: AS Adema 149-0 Stade Olympique L'Emyrne (Madagascar).Inatoka kwa mdau.
1995: Man Utd 9-0 Ipswich Town (Premier League record)
2001: Australia 31-0 American Samoa (World Cup qualifier)
2002: AS Adema 149-0 Stade Olympique L'Emyrne (Madagascar).Inatoka kwa mdau.
Comments