Na Martha Saranga Amini
Wakati mapigano yanaendelea Huko mashariki mwa Jamhuri Ya Kidemokrasia
ya Congo,DRC Watu wanaozungumza lugha ya Kinyarwanda al maarufu kama
Banyamulenge wamevilaumu vyombo vya usalama na raia kuendelea
kuwanyanyasa huku Viongozi wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini wakisema
watahakikisha usalama wa raia hao.
Baadhi wa wapiganaji waasi wa M23 wakiwa
kambini Rumangabo DRC waasi hawa wanatuhumiwa kukiuka haki za binadamu
kwa kuwatesa raia
Reuters/James Akena
Reuters/James Akena
Katika mazungumzo na Gavana wa Jimbo la Kivu ya Kaskazini raia hao
kutoka kabila la Banyamulenge waliilaumu serikali ya Rwanda pamoja na
waasi wa Kundi la M23,kutetea vita vya mashariki mwa Drc kuwa ni kwa
lengo la kusaka maslahi ya wanyarwanda.
Kwa upande wao Viongozi wa serikali pamoja na wale wa kijeshi wamesema
tayari wamefanikiwa kusuka mikakati iliyo thabiti ili kuhakikisha kwamba
usalama wa Banyamulenge unazingatiwa katika Jimbo nzima la Kivu ya
Kaskazini.
Hayo yanajiri wakati Hali ya wasi wasi inazidi kutanda katika mji wa
Kiwanja ulioko umbali wa kilomita takribani hamsini kaskazini mwa Jiji
la Goma ambapo imeripotiwa kuwa zaidi ya watu mia mbili waliozingirwa
Wakati wa Mkutano wa Hadhara ulioshikiliwa na M23 Alhamisi iliyopita
wanaendelea kushikiliwa,kupigwa na kuteswa katika Gereza la Nyongera.
Mashirika ya kimataifa na Asasi za kiraia Huko Kivu ya Kaskazini
yanasema kuna Hofu kwamba huenda baadhi ya Watu watakuwa wameuawa,au
kukumbwa na majeraha makali kufuatia Vichapo wanavyopigwa na Waasi
waM23.
Hata Hivyo M23 Hawajathibitisha wala kukanusha taarifa zinazohusiana na kukamatwa kwa watu katika Mji wa Kiwanja.
Via kiswahili.rfi.fr
Comments