“Nimefanya mapenzi na wanaume watano tofauti tokea niolewe miaka mitatu iliopita, mume wangu hajui chochote”
Najua story yangu itawafanya watu wengi wanifokee lakini nitashukuru kwa msaada wowote nitakaoupata.
Niliolewa na mume wangi April 2010. Ingawa kwa mara ya kwanza sikuwa
na nampenda mume wangu, lakini nilikuwa nazidi kuzeeka na sikuweza
kumpata mwanaumbe yeyote wa dini yangu na kabila langu, wazazi wangu
walinitambulisha kwa huyu mwanaume na kunilazimisha niolewe nae.
Mara ya kwanza natoka nje ya ndoa ilikuwa bahati mbaya. Nilikutana na
mpenzi wangu wa zamani na tukabadilishana Pins zetu za BlackBerry. Huwa
tunachat mara zote na nikaanza kutoifurahia ndoa yangu kwahiyo
nikamshawishi huyu ex wangu. Tukaanza kukutana na kuanza kufanya
mapenzi. Baadae akahamia kutoka huku mjini na kuhamia mji wa mbali na
hatimae mahusiano yetu yakaishia hapo.
Kutoka hapo nimekuwa na mahusiano na wanaume wengine wane ikiwemo
mume wa rafiki yangu. Nina watoto wawili na mume wangu lakini siridhiki
katika mapenzi.
Mume wangu ni mpole na ananipenda, na nimetokea kumpenda lakini
nashindwa kuacha mahusiano yangu ya nje ya ndoa. Kinachonisikitisha
zaidi ni kwamba mume wangu hajui chochote kile kinachoendelea. Simpi
nafasi yoyote ile ya kuwa na wasiwasi na mimi. Nafuta sms zote kwenye
simu yangu ingawa huwa hana tabia ya kuchungulia kwenye simu zangu.
Nahakikisha hagundui chochote kwasababu nataka familia yetu
isisambaratike.
Hivi karibuni nimeongea na mchungaji wangu ambaye amenishauri
niendelea kumwomba Mungu na kufunga lakini hii hainisaidii kwasababu
bado naendelea kutoka nje ya ndoa.
Najua natakiwa kuacha lakini sijui ni vipi. Tafadhali nisaidieni.
Kumsaidia Mke Wa Mtu Huyu katoe ushauri wako click hapa >> http://www.mapenziforums.com
Comments