Na Martha Saranga Amini
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis amewaunga mkono vijana
waliochukua hatua ya kuandamana kwa lengo la kutaka mabadiliko
akihutubia takribani watu milioni mbili huko Brazil.
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis akiwa Rio De Jeneiro,Brazili photo/dailymail
Papa Francis aliwaambia waumini wa kanisa Wakatoliki ambao wengi wao
walikuwa vijana waliokusanyika katika pwani moja huko Rio de Janeiro
kwamba alifuatilia habari duniani na kuona wimbi kubwa la vijana
likifanya maandamano kwa lengo la kueleza uhitaji wa haki na udugu.
Papa aliongeza kuwa Vijana wanaoonekana wakiandamana wameamua kuwa
watendaji wa mabadiliko na kuwataka vijana kuwajibika wanapoguswa na
masuala ya kijamii na kisiasa katika maeneo mbalimbali duniani.
Mamilioni ya waandamanaji walijitokeza katika maeneo mbalimbali nchini
brazil mwezi uliopita wakipinga ufisadi,matumizi mabaya ya mali ya
umma,na gharama kubwa za kufanyika kwa kombe la dunia mwaka 2014 nchini
humo maandamano ambayo mara zote huishia kuwa ghasia. Via kiswahili.rfi.fr
Comments