Ndugu zangu,
Inasemwa, kuwa kwenye mafanikio ya mwanamme nyuma yake kuna mwanamke. Dhana hii ina walakini, maana, hata hapa, kwenye mafanikio ya mwanamme, tunaamua kwa makusudi kumweka mwanamke nyuma.
Ni kwa nini mwanamke asiwe kando au hata mbele pale kwenye mafanikio ya mwanamme? Na mara nyingi huo ndio huwa ukweli, lakini, kwa makusudi ama kwa kutotambua, huwa tunaufumbia macho ukweli huo.
Ndugu zangu,
Naiangalia ziara ya Barack Obama Afrika na yale yenye kusemwa na kuandikwa. Nayaona mapungufu, yumkini yanatokana na mitazamo yetu inayotokana na makuzi yetu. Kwamba hata katika hili la mafanikio ya Obama, tunamwona mkewe, Michelle Obama, kuwa ni kiumbe aliye nyuma ya mafanikio ya mumewe, Barack Obama. Na tunapojaribu kumwangalia Michelle, basi, yanaandikwa yenye kuhusu urembo wake, ama mavazi na yale ya jikoni na... bofya chini usome zaidi...
Comments