Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya
kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki
mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.
MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan,
amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha
biashara ya dawa za kulevya.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan.
Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha.
“Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na
kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama
kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake
kwenye barua hiyo.
“Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa
hayupo nje ya nchi, kwani katika maelezo yake anataja jina la Balozi
Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete
alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa
Shirikisho la Ujerumani.
“Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani
hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernad na kukatwa kwa
wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye
uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo
tayari kujiuzulu ubunge wangu.
“Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni
lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu
waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu,” alisema Azzan.
Comments