Na Mahad Ibrahim, Mogadishu
Kikundi cha wataalamu cha al-Shabaab cha tawi la Amniyat kinaweza kuwa
kikosi cha mwisho kinachomuweka madarakani kiongozi wa kikundi cha
wanamgambo Ahmed Abdi Godane kwa vile kikundi kinaendelea kupoteza
maeneo na makamanda wapinzani wanashinikiza uasi wao dhidi ya utawala
wake, waangalizi wasema.
Picha iliyotumwa na al-Shabaab katika
akaunti ya Twitter tarehe 29 Aprili, ikiaminiwa kuonesha majeshi
waaminifu kwa Godane. [Jalada]
Wanachama wa Amniyat wamepata mafunzo na operesheni maalumu za hali ya
juu ambao kazi zao zinajumuisha kukusanya habari za kiintelijensia ili
kutekeleza misheni za mauaji na kulipua mabomu.
Muundo wa uongozi wa Al-Shabaab umegawika katika sehemu tatu: Jabhad,
tawi la kijeshi; Hizb, ni sawa na polisi; na Amniyat, kitengo cha
kiintelijensia, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Redio Mogadishu na aliyekuwa
msemaji wa Mahakama za Kiislamu Abdirahim Isse Addow.
Askari wapya mwanzoni hupewa mafunzo makambini, ambapo baadaye wakufunzi
huwapeleka katika moja ya matawi hayo, alisema. Amniyati pia huajiri
watendaji kutoka matawi mengine ndani ya al-Shabaab.
"Mtu ambaye ni mbunifu, shujaa, mwaminifu kwa emir [Godane] na itikadi
za kikundi, na anayeweza kutunza siri huchaguliwa kuwa mwanachama wa
Amniyat," Addow aliiambia Sabahi. "Baadaye hupewa mafunzo maalumu na
hutengwa katika vitendo tofauti kama vile kikosi cha ulipuaji mabomu na
mabomu ya kuzika ardhini, kitengo cha milipuko, kitengo cha mauaji, na
kitengo cha intelijensia.
Hata hivyo, Amniyat kimekuwa kikidhoofishwa na habari zinazotolewa na
waasi na wapiganaji waliokamatwa, Addow alisema. Kwa mfano, maafisa wa
usalama huko Puntland walimjeruhi na kumkamata kamanda wa Amniyat mwezi
wa Juni.
Comments