|
MAHAKAMA Ufaransa imemuagiza mwanasoka wa kimataifa wa Ivory Coast, Didier Drogba kulipa Euro 450,000 kwa kampuni ya ujenzi ya mjini Corsica baada ya kutoilipa kwa kumfanyia kazi mjini mjini Abidjan
Kampuni ya Acqua Viva ilimfikisha kortini mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea Mei kwa kugoma kulipa salio la malipo baada ya kujengewa nyumba ya kifahari iliyokamilika mwaka 2009.
Kampuni hiyo imelalamika pia wafanyakazi wake kuzuiwa kufika eneo la nyumba hiyo waliyojenga, kitu ambacho Jaji amesema si haki na kwamba kilitokana na maelekezo ya Drogba na mkewe, raia wa Mali, Lala Diakite.
Wakati mchezaji huyo wa zamani wa Marseille mwenye umri wa miaka 35, aliyejiunga na Galatasaray ya Uturuki mapema mwaka huu, ameamua kukata rufaa, lazima alipe fedha hizo mapema ili kutekeleza amri ya Mahakama. Chanzo: supersport (HM)
Comments