Majid Ahmed alichangia katika ripoti hii kutoka Mogadishu
Katika mfululizo wa ujumbe uliotolewa hivi karibuni kupitia Twitter,
al-Shabaab ilijisifu kuhusu namna wapiganaji wake walivyofanya
mashambulio zaidi ya 100 kwa kipindi cha nusu ya kwanza ya Ramadhan, na
kuapa kuongeza vurugu wiki zijazo.
Mwanamke wa Somalia akiruka juu ya maiti
iliyofunikwa baada ya bomu la kujitoa muhanga kulipuliwa na gari
iliyosheheni milipuko kwenye msafara wa vikosi vya Umoja wa Afrika huko
Mogadishu tarehe 12 Julai. [Mohamed Abdiwahab/AFP]
"Kati ya operesheni za kijeshi 108 zilizofanywa na HSM [al-Shabaab], 57
zilikuwa za mashambulio ya milipuko na maguruneti, 41 zilikuwa za
kukabiliana moja kwa moja na mashambulio ya kushtukiza," kikundi hicho
cha wanamgambo kilisema tarehe 24 Julai.
Al-Shabaab walisema pia walifanya mauaji kwa sababu za kisiasa tisa na
shambulio la kujitoa muhanga dhidi ya msafara wa Misheni ya Umoja wa
Afrika nchini Somalia (AMISOM) huko Mogadishu tarehe 12 Julai, ambapo
al-Shabaab walidai kuwajeruhi maofisa wa upelelezi wa Marekani.
Inadhaniwa kuwa "Shambulio la Ramadhan", kampeni ya al-Shabaab ya vurugu
"imejikita zaidi katika mji mkuu, na takriban nusu ya operesheni zote
za HSM zilifanyika huko Mogadishu".
Shabelle ya Chini & Jubba ya Chini pia zimeshuhudia vita vikali
wakati wa nusu ya kwanza ya Ramadhan, pamoja na idadi kadhaa ya
mashambulio kutarajiwa kuibuka ghafla," al-Shabaab alisema.
Katika ujumbe mbili uliotumwa tarehe 16 Julai, al-Shabaab ilielezea sababu zake za kufanya vurugu.
"Ramadhan ni mwezi wa Jihadi na kutoa sadaka. Ni muda wa kufanya vitendo
vya uadilifu na kutoa shukrani kwa Allah kwa huruma zake," ilisema. "Na
njia gani iliyo nzuri ya kufunga Ramadhan na kutoa shukrani kwa Allah
kuliko kuchapa shingo za wavamizi na kuharibu matamanio yao!"
Katika jaribio la kuonyesha umoja kukiwa na mgawanyo wa ndani
unaoendelea, al-Shabaab ilisema tarehe 24 Julai, "Kama kuna chochote,
kinachoibuka haraka katika mashambulio yaliratibiwa ni kipimo bayana cha
uimara cha Mujahidina na uwezo wao wa uendeshaji."
Comments