Ramadan Kareem ndugu zangu Waislam, niwatakie mwezi mtukufu mwema .
Ndugu zangu watanzania mashabiki wa
soka mara nyingi naweza kuwa na mtazamo wa peke yangu na wakati mwingine
nisiwe na mtu wa atayeona nipo sahihi kwa mfano zipo njia mbili za
kuishi. " Moja ni hakuna kitu kilicho miujiza na nyingine ni kwamba kila kitu ni miujiza" sijui hapo katika soka leo tutumie njia ipi?
Mechi ya mchujo ya Kombe la Afrika kwa
Wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN) kati ya Tanzania, Taifa Stars na
Uganda, The Cranes itakayochezwa Jumamosi (Julai 13 mwaka huu) kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mechi hii ni muhimu kwa timu yetu
siombei tufungwe ila naona kabisa dalili za kufungwa sioni mipango
yoyote madhubuti zaidi ya kusikia matangazo ya viingilio vya mlangoni
kutoka kwa wenye mamlaka na soka la Tanzania .
Sina cha kumalizia, Niwatakie Siku njema
Capt Mkami Jr
Comments