Tafiti nyingi zinaonesha kuwa watu wengi walio funga ndoa wamewapiku
wale wasio funga ndoa kwenye umri wa kuishi. Watafiti hawa wamebainisha
kuwa mfumo wa maisha wa mtu aliye kwenye ndoa huchangia mabadiriko yake
kifikira na hata kiuchumi hivyo kwa njia moja au nyingine ndio sababu ya
wale walio kwenye ndoa kuishi kwa muda mrefu.
Wakati ndoa huchangia kuongea muda wa kuishi na faida nyingine nyingi
kwenye afya ya binadamu, tafiti zinaonesha kuwa wale walio achika /
tengana au wajane umri wao wa kuishi huwa mfupi kuliko wale wasioolewa
/oa kabisa.
Je unataka kupokea dondoo za kila siku kwenye email yako, jiunge na mlisho wa dondoo za afya toka TanzMED kwa kwenda HAPA
Comments