MKUU wa Jeshi la Misri amewataka wananchi kujitokeza kuandamana siku ya Ijumaa dhidi ya kile anachokiita ugaidi.
Abdel Fattah al-Sisi amesema anawataka watu kuunga mkono jeshi na kulikabidhi jukumu la kukabiliana na ghasia pamoja na ugaidi.
Wafuasi wa Mohammed Morsi aliyeondolewa mamlakani na jeshi, wamekuwa wakiandamana dhidi ya jeshi ambalo lilimuondoa mamlakani tarehe 3 mwezi Julai.
Lakini Generali Sisi alisema wito wake sio wa ghasia bali anataka kuwepo maridhiano ya kitaifa. (HM)
Soma zaidi...

Comments