Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla. MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan. Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha. “Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo. “Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa ...