Muigizaji wa filamu Riyama Ally, amesema anamuunga mkono mwenzake
Wema Sepetu katika juhudi zake za kusaka ubunge katika uchaguzi mkuu wa
mwaka huu.
Wema alimwambia Mwandishi wa Habari hizi kuwa, endapo akiingia
Bungeni atakuwa msaada mkubwa kwa wasanii na tasnia ya sanaa kwa ujumla.
Aliwashauri wasanii wa kike na wengine kumuunga mkono katika harakati zake za kutimiza ndoto hiyo.
“Tuungane kwa pamoja kumsaidia aweze kutimiza ndoto yake akifanikiwa
atakuwa msaada mkubwa katika tasnia ya sanaa kwa sababu anafahamu
mahitaji ya wasanii,” alisema.
Comments