Kamshina wa TRA ameliagiza Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)
kupitia kwa katibu mkuu wake kuwa, vilabu vyote vya mpira wa miguu
nchini vinavyoajiri walimu, wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi
wahakikishe wanaweka kipengele cha kodi katika mikataba wanayoingia
kuwaajiri.
Vilbu vya vinapaswa kuwasilisha mikataba yote ya ajira ya wachezaji
na walimu wao ili kukokotoa kodi stahiki kwa kila mmoja wao na mikataba
yao kugongwa muhuri na stempu.
Kwa mujibu wa sheria za Kodi ya Mapato ya mwaka 2004, kufungu namba
7, kila mtu anayepata mapato yatokanayo na ajira katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania anawajibika kulipa kodi ya mapato kulingana na
kipato chake.
Aidha kwa mujibu wa Sheria ya Ushuru wa stempu ya mwaka 1973, kifungu
namba 5 kikisomwa pamoja na jedwali la sheria hii, kila mkataba
unatakiwa kugongwa muhuri na stempu na ofisa wa stempu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania.
Kwa kuwa TFF ndio mlezi na msimamizi mkuu wa vilabu vya Mpira wa
Miguu hapana nchini na hasa Ligi Kuu, tunaviomba vilabu vyote
kuhakikisha vinawasilisha mikataba ya walimu na wachezaji yao ofisi za
Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa ajili ya kugongwa mihuri na stempu.
Comments