Shirikisho la mpira la Brazil limekubaliana na adhabu aliyopewa
nahodha wa timu hiyo Neymar ya kusimamishwa kucheza mechi nne, Neymar
alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo wao dhidi ya Colombia kutokana na
kitendo chake cha kumpiga na mpira mchezaji Pablo Armero pamoja na
kumpiga kichwa mchezaji mwingine aliyejaribu kumzingira.
Taarifa iliyotolewa leo na shirikisho hilo imebainisha kuwa uamuzi wa kutokata rufaa dhidi ya adhabu hiyo ulichukuliwa jana baada ya mkutano kati benchi la ufundi la timu hiyo pamoja na mchezaji mwenyewe.

Hapo kabla kocha mkuu wa kikosi hicho Dunga alikaririwa akisema kuwa
shirikisho hilo linafikiria kukata rufaa kupinga adhabu hiyo.
Comments