Msanii mkongwe wa filamu nchini, Juma Ally Salim ‘Mzee Kankaa’
amefariki dunia leo alfajiri akiwa nyumbani kwake Tandale jijini Dar es
Salaam baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu.juma
Mwili wa Mzee Kankaa unatarajiwa kuzikwa leo saa 10 jioni katika makaburi ya Ali Maua jijini Dar es Salaam.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi kwa zaidi ya
miaka mitatu. Msiba upo nyumbani kwa marehemu eneo la Tandale-Chama
jijini Dar.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN!
Chanzo: GPL
Comments