Tume ya Uchaguzi ya Burundi imepanga Julai 15 kuwa tarehe mpya kwa ajili ya uchaguzi wa utata wa urais.
Tarehe hiyo iliyopendekezwa imekuja baada ya wito uliofanywa na
viongozi wa kanda kuchelewesha uchaguzi huo, ambapo awali ulipangwa Juni
26, angalau wiki sita zimesogezwa mbele.
Burundi ilikumbwa na maandamano na mapinduzi yaliyoshindikana
kumuondoa Rais Pierre Nkurunziza aliyetangaza kuwania muhula wa tatu
mwezi Aprili.
Anahitaji kuthibitisha tarehe mpya kabla ya uchaguzi huo kufanyika.
Nkurunziza amekataa wito wa kutogombea tena. Pamoja na wahisani wa
Magharibi kukata baadhi ya misaada kwa taifa hilo maskini Afrika.
Comments