Diego Maradona anataka kuwania urais wa FIFA kuchukua nafasi ya Sepp Blatter, kwa mujibu ripoti za Amerika ya Kusini.
Maradona, 54, amekuwa mkosoaji mkali wa Blatter, nahodha huyo wa
zamani wa Argentina na kocha wa ameamua kuwania nafasi hiyo na kuwa mtu
mwenye nguvu katika soka duniani, mtangazaji na mwandishi wa Uruguay
Victor Hugo Morales alisema.
Morales, maarufu kwa maoni yake ya goli la ajabu la pili Maradona
dhidi ya Uingereza kwenye robo fainali ya Kombe la Dunia 1986, alisema
kwenye Twitter kuwa ameambiwa na Maradona kutoa taarifa hizo.
Comments