Umoja wa watendaji wakuu wa kampuni wa CEO RoundTable (CEOrt)
umeandaa mdahalo wa kuzungumzia mbio za urais utakaowahusisha viongozi
wa vyama vya upinzani, Profesa Ibrahim Lipumba, Dk Willibrod Slaa, Zitto
Kabwe na Emmanuel Makaidi, lakini Chadema imesema itakuwa tayari kwa
midahalo baada ya mchakato wa ndani kukamilika.
Kauli hiyo ya Chadema inaweza kuwa kikwazo kingine kwa CEOrt
kuendesha midahalo hiyo baada ya wa kwanza uliokuwa uhusishe makada 10
wa CCM wanaoomba ridhaa ya chama hicho kuwania urais, kushindwa
kufanyika kutokana na viongozi wa sekretarieti kutoa kauli tofauti siku
moja kabla.
Kiongozi wa CEO, Ali Mufuruki alisema jana kuwa Dk Slaa, Profesa
Lipumba, Makaidi na Zitto, ambaye ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo,
wamethibitisha kushiriki kwenye mdahalo huo utakaofanyika kesho kuanzia
saa 1:00 jioni jijini Dar es Salaam.
Lakini Dk Slaa aliiambia Mwananchi jana kuwa Chadema itakuwa tayari
kushiriki kwenye midahalo baada ya kumaliza mchakato wa kupata mgombea
wake na kukamilisha Ilani ya Uchaguzi, mambo ambayo alisema hupitishwa
na vikao vya juu.
“Kamanda, sijui kama ni kongamano au mdahalo: 1. Chadema inaendeshwa
kwa katiba, kanuni na taratibu zake. Hadi siku ya leo taratibu zetu
hazijafikia kupata aspirants (watangazania),” alisema katibu huyo mkuu
wa Chadema katika ujumbe wake mfupi wa simu.
“2. Kama kuna waliopata aspirants, Chadema bado mchakato wetu
unaendelea. 3. Midahalo inafanywa kwa msingi wa ilani. Chadema ilani
yetu haijafika bado mbele ya vikao vya maamuzi, yaani Baraza Kuu na
Mkutano Mkuu. Hivyo tukienda mdahalo tutakuwa tunazungumzia ilani ipi?
“Hivyo tuko tayari kwa midahalo yote baada ya mchakato wetu wa ndani kukamilika.”
Mufuruku alikuwa ametuma taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook
na alipopigiwa simu na Mwananchi, alithibitisha kuwapo kwa mdahalo huo
ambao alisema utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni, redio
na intaneti.
Kuhusu ushiriki wa Zitto, ambaye atagombea ubunge wa Jimbo la Kigoma
Mjini, Mufuruki alisema CEOrt imemualika kwa kuwa ni kiongozi wa chama
ambacho kinaweza kusimamisha mgombea wa urais.
“Kushiriki si lazima uwe unachukua fomu za kugombea urais. Yeye ni
kiongozi wa chama ana mawazo yanayoweza kutoa mchango kwenye mdahalo,”
alisema Mufuruki.
CEOrt imepanga kufanya midahalo kadhaa mwezi huu na Juni 25
itaendesha mdahalo utakaoshirikisha wagombea kutoka CCM baada ya kada
mmoja tu, Balozi Amina Salum Ali, kujitokeza kwenye mdahalo wa kwanza na
hivyo kusababisha uahirishwe.
Profesa Lipumba, ambaye amechukua fomu za kuomba ridhaa ya CUF
kupitishwa kugombea urais kwa mara ya tano iwapo jina lake litapitishwa
na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), aliiambia Mwananchi jana kuwa
atashiriki kwenye mdahalo huo, kama ilivyo kwa Makaidi ambaye
amepitishwa na NLD kuwania nafasi hiyo.
NCCR-Mageuzi, Chadema, CUF na NLD vimepanga kusimamisha mgombea mmoja
atakayeungwa mkono na vyama vyote, lakini kila chama kitalazimika
kupata mgombea wake ambaye jina lake litapelekwa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kupitishwa kabla ya kuteua mmoja ambaye
atawakilisha vyama hivyo kwenye Uchaguzi Mkuu.
ridhaa ya chama hicho kuwania urais, kushindwa kufanyika kutokana na
viongozi wa sekretarieti kutoa kauli tofauti siku moja kabla.
Kiongozi wa CEOrt, Ali Mufuruki alisema jana kuwa Dk Slaa, Profesa
Lipumba, Makaidi na Zitto, ambaye ni kiongozi mkuu wa ACT-Wazalendo,
wamethibitisha kushiriki kwenye mdahalo huo utakaofanyika kesho kuanzia
saa 1:00 jioni jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo, Dk Slaa aliliambia gazeti hili jana kuwa, Chadema itakuwa
tayari kushiriki kwenye midahalo baada ya kumaliza mchakato wa kupata
mgombea wake na kukamilisha ilani ya uchaguzi, mambo ambayo alisema
hupitishwa na vikao vya juu.
“Kamanda, sijui kama ni kongamano au mdahalo: 1. Chadema inaendeshwa
kwa katiba, kanuni na taratibu zake. Hadi siku ya leo taratibu zetu
hazijafikia kupata aspirants (watangazania),” alisema katibu huyo mkuu
wa Chadema katika ujumbe wake mfupi wa simu.
“2. Kama kuna waliopata aspirants (watiania), Chadema bado mchakato
wetu unaendelea. 3. Midahalo inafanywa kwa msingi wa ilani. Chadema
ilani yetu haijafika bado mbele ya vikao vya maamuzi, yaani Baraza Kuu
na Mkutano Mkuu. Hivyo tukienda mdahalo tutakuwa tunazungumzia ilani
ipi?
“Hivyo tuko tayari kwa midahalo yote baada ya mchakato wetu wa ndani kukamilika.”
Mufuruki alikuwa ametuma taarifa hiyo kwenye ukurasa wake wa facebook
na alipopigiwa simu na Mwananchi, alithibitisha kuwapo kwa mdahalo huo
ambao alisema utaonyeshwa moja kwa moja na vituo vya televisheni, redio
na intaneti.
Kuhusu ushiriki wa Zitto, ambaye atagombea ubunge wa Jimbo la Kigoma
Mjini, Mufuruki alisema CEOrt imemualika kwa kuwa ni kiongozi wa chama
ambacho kinaweza kusimamisha mgombea wa urais.
“Kushiriki si lazima uwe unachukua fomu za kugombea urais. Yeye ni
kiongozi wa chama ana mawazo yanayoweza kutoa mchango kwenye mdahalo,”
alisema Mufuruki.
Chanzo: Mwananchi
Comments