Msanii wa filamu, Esha Buheti amekuwa kwenye wakati mgumu mara baada
ya kupokea habari mbaya zilizompelekea kwenda kupima ugonjwa wa ukimwi.
Amefanya hivyo baada ya kusikia maneno kwa watu kwamba mpenzi wake ana michepuko mingi.
Mwigizaji huyo alisema, baada ya kupata taarifa hizo, ndipo alitaka kujua afya yake mapema.
“Nilivyopima na kukutwa nipo salama nilifurahi sana hata kama
nisingekuwa salama, ningejitangaza kwa sasa ninachokifanya ni kuwa
muaminifu na kuwahamasisha wenzangu kupima, “alisema
Alisema kuwa anapenda kuwaasa wasanii wezake pamoja na jamii kuweza kupima na kujua afya zao.Inatoka kwa mdau
Comments