Salim Kikeke
Sergio Ramos anayesakwa na Manchester United anataka kuondoka Real Madrid baada ya klabu hiyo kushindwa kukanusha uvumi wa uhamisho wake uliotajwa na mgombea urais wa Barcelona Jordi Maji (AS), Liverpool wameongeza dau lao kufikia pauni milioni 16 kumtaka kiungo mkabaji wa Real Madrid Asier Illarramendi, 25 (Marca), Liverpool pia wanamfuatilia mshambuliaji wa Sevilla Carlos Bacca, 28, na Salomon Rondon, 25, wa Zenith St Petersburg iwapo watashindwa kumpata Christian Benteke, 24 (Liverpool Echo), meneja wa Liverpool Brandan Rodgers anataka kununua wachezaji watatu, Illarramendi, Bacca na Rondon kwa mkataba utakaofikia pauni milioni 75 (Daily Star), West Ham wanataka kumsajili Moussa Dembele, 27, kutoka Tottenham kwa pauni milioni 12. Chelsea pia wanamtaka Mbelgiji huyo (Sun), West ham wana imani kuwa kitita cha pauni milioni 14 kitaweza kusababisha uhamisho wa mshambuliaji wa Marseille Dimitri Payet, 28 (Guardian), kipa wa Chelsea Petr Cech, 33, amefikia makubaliano ya maslahi binafsi ya Arsenal, lakini timu hizo mbili bado hazijakubaliana ada ya uhamisho (Sky Sports), winga wa Tottenham, Andros Townsend huenda akachukuliwa na Sunderland (Newcastle Chronicle), Tottenham huenda wakapata hasara ya pauni milioni 15 kwa Roberto Soldado baada ya kuanza mazungumzo na Galatasaray kumuuza mshambuliaji huyo kwa pauni milioni 11 (Daily Mirror), Raheem Sterling alisafiri kwa ndege ya kukodi kutoka likizo yake Ibiza wakati Manchester City wakiongeza dau lao kufikia pauni milioni 50 (Daily Mail), mshambuliaji wa Porto Jackson Martinez, 28, anasubiri Arsenal wachukue hatua za kumsajili baada ya kukataa nafasi ya kuhamia AC Milan (Daily Express), Ronald Koeman anajiandaa kuvunja rekodi ya uhamisho ya Southampton kwa kutoa pauni milioni 15 kumsajili beki wa Atletico Madrid, Toby Alderweireld, 26. Beki huyo ana thamani ya pauni milioni 18 (Daily Mirror), kiungo wa Juventus Andrea Pirlo, 36, ataungana na Frank Lampard, New York City FC (Goal.com), bodi ya Crystal Palace iko tayari kuzuia hatua ya Alan pardew kumsajili Charlie Austin, 25, kwa sababu hawataki kulipa pauni milioni 15 (Daily Mirror), Southampton pia wanamtaka Austin, anayesakwa pia na Liverpool na Chelsea (Daily Express), baada ya kushindwa kumsajili Jackson Martinez, AC Milan bado wanataka mshambuliaji mzuri, meneja Adriano Galliani akiwa tayari kutoa euro milioni 50-55 kumsajili Edinson Cavani, na hata Zlatan Ibrahimovic (Corriere dello Sport), Chelsea wameongeza kasi na kuwapiku West Ham katika kumsajili kiungo Alex Song (Daily Express), Chelsea wanaonekana kupoteza nafasi ya kumsajili Axel Witsel, huku mchezaji huyo wa Zenith akikaribia kujiunga na AC Milan. Manchester United pia walikuwa wakimtaka mbelgiji huyo ambaye anakaribia kwenda San Siro kwa pauni milioni 21 (Gazzetta dello Sport), Manchester United wana matumaini ya kuishawishi Glatasaray kumchukua kipa Fernando Musrela. Man Utd, wapo tayari kumtoa Antonio Valencia katika mkataba huo (Fanatik), Fernabahce bado wanataka kumsajili Robin van Persie, baada ya Galatasaray kuacha kumfuatilia (Daily Mirror). Habari za uhamisho zilizothibitishwa, nitakujulisha zitakapothibitishwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!!!
kutoka Facebook
Comments