Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta
Waziri wa
Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasimama kifua mbele kupambana na
rushwa kwa kuwa aliwahi kuikataa rushwa ya Dola 70,000 (sawa na
Sh140,000) milioni).
Sitta
alisema hayo jana wakati akizungumza na makada wa chama hicho
waliojitokeza kumdhamini katika wilaya ya Geita mkoani Geita na kusema
kuna baadhi ya watia nia wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais
watapambana na rushwa wakati ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala
rushwa. Viwango vya kubadili fedha za kigeni, kwa sasa Dola moja ya
Marekani sawa na Sh2,000.
“Nilitumwa
Canada kutafuta ndege tatu, jioni moja tukiwa Canada tunajiandaa
kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni tuliyonunua ndege,
akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege zetu
zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela
tuzipeleke benki gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.
“Watazameni
hawa watu... mtu kawa waziri mwaka mmoja leo anataka urais, halafu
anasema atapambana na rushwa...utapambana na rushwa wapi wakati hata
hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa makini, mtawajua tu kwa
macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli,” alisema.
Aliendelea, “Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego wa
shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na
wakubwa zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani
wa ndege.”
Sitta
aliwataka wananchi hao kuwatazama kwa makini watangaza nia hao, na
kuwauliza iwapo tayari walishawahi kupambanishwa na rushwa.
Lowassa aonya kuhusu viongozi wanafiki
Kigoma.
Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuwa makini na kauli za baadhi ya viongozi
wa Serikali wanaojinadi kwa kusema wanawapenda Watanzania maskini,
lakini mioyoni mwao hawana huruma.
Hayo yalisemwa na Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alipokuwa akitafuta wadhamini
mkoani hapa, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu zenye majina ya wanachama waliojitokeza kumdhamini.
Akiwa
katika ofisi ya CCM mkoa, Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji
Kubaji alimkabidhi Lowassa fomu 45 za wana CCM waliomdhamini.
“Wapo
viongozi, wanajifanya wanawapenda na kuwajali watu masikini, lakini wao
wenyewe unawakuta ni matajiri, hawa jamaa ni waongo sana hawa,” alisema.
Lowassa
aliwataka wakazi Kigoma kumuombea ili dua na sala zao ziweze kumsaidia
afikie malengo aliyojiwekea. “Nina dhamira ya kuwatumikia, lakini lazima
mniombee sana dua na sala ili mambo yangu yaende vizuri hatimaye
nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi nachukia sana umaskini, kwa hiyo
lazima tuwe kama Malaysia ambayo kiongozi wake alipambana kuhakikisha
wananchi wanaondokana na umaskini,” alisema.
Wasira awashangaa wanaotumia matarumbeta
Waziri wa
Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira amesema anashangazwa na
baadhi ya wagombea wenzake, wanaokwenda kutafuta wadhamini kwa
matarumbeta na miziki ya kuwaita wananchi.
Wasira
alitoa kauli hiyo mjini Musoma katika Ofisi ya CCM Mkoa, Adamu Ngalawa
wakati alipokuwa akipokea majina na kadi za wadhamini waliojitokeza
kumdhamini.
Alisema
wagombea wanaofanya hivyo wanakiuka taratibu, kanuni, sheria na katiba
za chama kwa kuwa chama hicho tawala kilishapitisha kuwa wakati wa
kutafuta wadhamini hakuna mgomWbea kuhutubia mkutano wa hadhara.
“Kuna
wagombea wanaitisha mkutano wa hadhara na kuwaita wananchi wakati hawana
cha kuwahutubia kwa kuwa wamezuiliwa kufanya hivyo...wanabaki
wakiwaeleza wananchi mniombee, wawaombee nini? Mimi nimeshatembea mikoa
zaidi ya 20 na hakuna sehemu nimewaita wananchi tofauti na kutoa taarifa
kwenye chama ili wadhamini niwapate,” alisema.
Wasira
alisema mkoa wa Mara una wagombea wanne wanaowania urais, lakini hakuna
atakayejitoa kwa misingi ya kuachiana kura kwa sababu hakuna mwananchi
wa kawaida atakayepiga kura bali maamuzi yatafanywa na Kamati Kuu ya
CCM.
Chanzo:Mwananchi
Comments