Usajili
wa wachezaji kwa hatua ya kwanza msimu huu (2015/2016) unaanza leo hadi
Agosti 6 mwaka huu wakati kipindi cha kutangaza wachezaji walioachwa au
kusitishiwa mikataba ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu.
Kipindi
cha kwanza cha uhamisho wa wachezaji ni kuanzia Juni 15 mwaka huu hadi
Julai 30 mwaka huu ambapo kupitia majina na kutangaza pingamizi ni kati
ya Agosti 7 na 14 mwaka huu huku Kuthibitisha usajili hatua ya awali ni
Agosti 15 hadi 19 mwaka huu.
Usajili hatua ya pili utakuwa kati ya Agosti 17 na Septemba 8 mwaka
huu ambapo kupitia na kutangaza majina ya pingamizi hatua ya pili ya
usajili ni kuanzia Septemba 8 hadi 14 mwaka huu huku uthibitisho wa
usajili hatua ya pili ni Septemba 15 na 17 mwaka huu.
Wachezaji wanaotoka nje ya Tanzania, usajili wa mtandao wa FIFA wa
TMS utakuwa wazi kuanzia leo hadi Septemba 6 mwaka huu ambapo klabu
zinazosajili wachezaji kutoka nje zinatakiwa kufanya hivyo kupitia
akaunti zao za mtandao wa TMS.
Kwa klabu ambazo hazina akaunti ya TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo ya TMS, na baadaye kuombewa akaunti hizo FIFA.
Kwa klabu ambazo hazina akaunti ya TMS zinatakiwa kuwasiliana na TFF ili mameneja wao wa usajili wapatiwe mafunzo ya TMS, na baadaye kuombewa akaunti hizo FIFA.
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inatarajiwa kuanza Agosti 22
mwaka huu, na ratiba inatarajiwa kutoka mwezi mmoja kabla ambapo ni
Julai 22 mwaka huu.
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Septemba 12 mwaka huu,
wakati Ligi Daraja la Pili (SDL) inatarajia kuanza Oktoba 17 mwaka huu.
Comments