Skip to main content

Nyota mpya klabu ya Yanga , Busungu afunguka “Nitapanda daladala nikipenda mwenyewe”




Gari mpya ya mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu
Gari mpya ya mshambuliaji wa Yanga Malimi Busungu
Uongozi wa klabu ya Yanga umemkabidhi gari mpya aina ya Toyota IST mshambuliaji wao mpya Malimi Busungu kutokana na makubaliano ya mkataba wao.
Mshambuliaji huyo wakati akiongea na mwandishi wa habari hii alisema kuwa “Nashukuru Mungu gari langu nimeshapewa na sasa napiga nalo misele na ukinikuta kwenye daladala basi nimependa mwenyewe au kuna tatizo, kazi iliyobaki ni kuthibitisha thamani yangu kwa Yanga,” alisema Busungu.
Mshambuliaji huyo amejiunga na mabingwa hao wa ligi kuu wiki chache zilizopita akitokea kwenye klabu ya Mgambo JKT ya jijini Tanga ambapo alimaliza ligi akiwa mfungaji bora wa klabu hiyo.
Sources: Shaffihdauda.com

Comments