Rapa anayejulikana kwa jina la The Game amekamatwa kwa kuhusika na
tukio la vurugu akiwemo polisi asiyekuwa kazini katika mechi ya mpira wa
kikapu mwezi Machi.
Afisa polisi wa Los Angeles Mike Lopez anasema Jayceon Terrell Taylor
(The Game), 35, alijisalimisha polisi kwenye idara ya Hollywood
Division mchana Jumatatu.
Taylor anatuhumiwa kumrushia ngumi afisa, tukio lilinaswa na kamera na kuwekwa mtandaoni.
Lopez anasema Taylor alifunguliwa mashtaka kwa kushukiwa kufanya
vitisho vya kihalifu. Baadae alitolewa kwa dhamana ya dola 50,000.
Comments