kerr (kushoto)
Kocha
mpya wa Simba, Dylan Kerr ametua leo mchana jijini Dar es salaam tayari
kuanza kazi ya kuiandaa timu kwa ajili ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Kocha mpya wa Simba akiongea na waandishi
Kerr,
raia wa Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira
wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali
duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na
Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.
Kerr
pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya
kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na South
Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini
Kerr
ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la
soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya
michezo.
Comments