Pamoja na msimu kuisha bila hata ya medali, United imewazidi magwiji wa Ulaya na kuwa juu kwenye The Brand Finance Football 50, kwa mujibu wa tafiti iliyoachiwa Jumatatu.
Mashetani wekundu kwa sasa ina thamani ya zaidi ya dola bilioni 1.2, ikiwa zaidi ya dola milioni 300 kwa Bayern Munich. Real Madrid, Manchester City na Chelsea zote zipo tano bora.
Ushindi wa Barcelona dhidi ya Juventus kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa siku ya Jumamosi uliwaongezea sola milioni 28 kwenye timu yao, lakini haikuwafanya kuwa juu ya City na Chelsea .
Mkurugenzi wa Brand Finance David Haigh alisema: “Mafanikio ya Manchester yamesababishwa na Ed Woodward, Cristiano Ronaldo wa upande wa soka la biashara.”
Comments