Rais Omar al Bashir wa Sudan
Rais Omar al Bashir wa Sudan ameondoka nchini Afrika Kusini.
Rais
Bashir ameondoka akiandamana na waziri wa maswala ya kigeni wa Sudan
huku ikiahidiwa kuwa watazungumza na waandishi wa habari pindi
watakapotua mjini Khartoum.
Mwandishi
wa BBC aliyeko Afrika Kusini Nomsa Maseko, anasema kuwa ndege ya rais
al Bashir ilijazwa mafuta jana usiku na kuwekwa mstari wa mbele tayari
kabisa kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi.
Rais Bashir amekuwa nchini Afrika kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.
Rais Bashir ameondoka licha ya kuwepo amri ya mahakama ya kumzuia kuondoka nchini humo hadi kesi dhidi yake itakaposikizwa.
Mahakama
hiyo ilikuwa inapaswa kuamua ikiwa Bwana al-Bashir atakabidhiwa kwenye
mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC yenye makao yake mjini
Hague Uholanzi ilikukabiliana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji
yahalaiki yanayomkabili .
Majaji watatu walikuwa wanasikiza kesi hiyo rais Bashir alipopuzilia mbali amri hiyo na kuondoka.
Rais Bashir anasakwa na mahakama ya ICC kujibu tuhuma za mauaji ya halaiki katika jimbo la Darfur
Rais huyo wa Sudan amekuwa nchini Afrika kusini kuhudhuria kikao cha viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.
Waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Ibrahim al-Ghandour, amesema Bwana al-Bashir atarejea Sudan baada ya mkutano huo.
"Tupo hapa kama wageni waalikwa na serikali ya Afrika Kusini.
Rais Bashir alikuwa huko kwa mualiko wa rais Zuma
ma''Naamini
serikali ya Afrika Kusini itaweza kukabiliana na mahakama zake na
yeyote anayejaribu kumzuia Rais Bashir kuondoka nchini humu.''
''Naweza
kuwaambia waziwazi kuwa Rais Bashir ataondoka kwa wakati kama ilivyokuwa
imepangwa." anasema waziri huyo wa mambo ya nje wa Sudan.BBC
Comments