Staa
wa Muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga ‘Linah’ akiwa ameketi na
William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’
kiukoo.
MREMBO anayefanya poa
kunako Bongo Fleva, Estelinah Sanga ‘Linah’, anadaiwa ‘kujiegesha’
kimahaba kwa shemeji yake Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ aitwaye
William Bugeme ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka wa Zarina Hassan ‘Zari’
kiukoo.
Ndani ya Ukumbi wa Triple 7
uliyopo Kawe jijini Dar hivi karibuni, paparazi wetu aliwaona wakiingia
sambamba na kukaa beneti kama mtu na mpenzi wake jambo lililozua
maswali kibao kutoka kwa wateja waliokuwepo ukumbini hapo.
Linah na Boss Mtoto katika pozi la kimahaba.
Mbali na kunaswa siku hiyo,
pia paparazi wetu amekuwa akiwashuhudia mara kadhaa wawili hao wakiwa
pamoja katika kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar.
Mara ya mwisho, Linah na
Boss Mtoto walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo za Kili Music
zilizofanyika ndani ya Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, mapema mwezi
huu.
Ndani ya Triple 7, paparazi
wetu aliamua kumfuata Linah ili ajiridhishe uwepo wake na mwanaume huyo
ambapo msanii huyo alijing’atang’ata na kusema:
“Huyu ni mtu wangu huwa
natoka naye. Sijui umenielewa? Natoka naye sehemu mbalimbali.Ila kukutoa
wasiwasi tambua kwa sasa sina mpenzi na nina haki ya kuwa naye, sina
mpaka wa kujiachia na Boss Mtoto,” alisema.
Comments