Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo. Lakini hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa kampuni ya magari ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia katika soko. Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000. Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?. Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo. Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata fedha kutokana na kilimo na uchimbaji. Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero. ...