Jumapili ya September 28 ilikuwa ni siku ya kuzaliwa mrembo aliyebeba taji la Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu. katika kusheherekea siku hiyo mpenzi wake Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz alithibitisha kwa vitendo kuwa mapenzi yao bado yako imara, kwa kumnunulia zawadi ya gari jipya aina ya Nissan. Picha ya gari hilo la rangi nyeusi iliambaatana na ujumbe mzuri ambao Diamond alimwandikia wema kupitia akaunti yake ya Instagram yenye followers 236,841. “Nlitama nikupe vingi, wenda ingenisaidia kueleza ni kias gani napenda nikuone ukifurahi kwenye siku yako hii ya kuzaliwa…lakini tu sina uwezo huo mumy… tafadhari pokea kidogo hichi nlichojaaliwa leo….” Huku akionesha gari hilo pichani