Walimu wa shule za sekondari na taasisi za juu nchini Kenya wameanza rasmi mgomo wao wa kitaifa hii leo baada ya kukosa kuafikia mwafaka na serikali kuhusu kutengewa pesa za kuwalipa marupurupu.
Mgomo huu unakuja baada ya kusomwa kwa bajeti ya serikali wiki jana. Walimu hao wanalalamika kuwa serikali imetenga mabilioni ya pesa kwa ununuzi wa vipakatilishi kwa wanafunzi wa darasa la kwanza badala ya kutumia pesa kwa miradi mingine ambayo ni muhimu zaidi katika sekta ya elimu.
Comments