Na Abdi Moalim, Mogadishu
Serikali ya Somalia inalazimika kufanya utafiti wa kina kuhusu athari za
matumizi ya tumbaku kwani Wasomali wengi hawana uelewa kuhusu madhara
ya kimwili na kiuchumi ya uvutaji, mtaalamu wa afya na maofisa wa ajira
wasema.
Faisal Aadan (kushoto), mwenye umri wa miaka 29 mkaazi wa wilaya ya
Weyne ya Mogadishu, alisema hajaajiriwa lakini hutafuta njia za kuweza
kuhimili tabia yake ya kupata pakiti la sigara kwa siku. [Dahir
Jibril/Sabahi]
Utafiti rasmi ungetoa mwanga kuhusu matatizo ya kiafya yanayohusiana na
uvutaji sigara na uhusiano kati ya uvutaji na masuala ya kifedha na
kijamii, alisema Adam Haji Ibrahim, daktari na mtaalamu wa afya ya jamii
ambaye anafundisha Chuo Kikuu cha Benadir.
Utafiti unahitajika pia kutambua idadi ya Wasomali wanaovuta, alisema.
"Hakuna utafiti wa kutumainiwa kuhusu idadi ya watu wanaovuta sigara,
matatizo yanayosababishwa na sigara kwao na hatari za jumla za kuvuta
kwa umma wa Wasomali," Ibrahim aliiambia Sabahi, akiongezea kwamba
kukosekana kwa serikali madhubuti inayoweza kutoa huduma za jamii za
jumla kwa raia wao kwa kipindi cha miaka 22 ndicho cha kulaumu.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, ambalo linahamasisha siku ya
Dunia isiyo na matumizi ya Tumbaku tarehe 31 Mei, takribani watu milioni
sita hufa kila mwaka kutokana ma matumizi ya tumbaku na zaidi ya watu
600,000 hufa kutokana na kuvuta moshi wa mtu anayevuta.
Comments