Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Pandu Ameir Kificho akiongoza Kikao
cha asubuhi cha maswali na majibu yalioulizwa na Wajumbe wa Baraza leo
asubuhi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakiwa katika Kikao cha asubuhi cha Maswali na Majibu leo
Waziri wa Nchi Ofisi Rais Ikulu Dkt. Mwinyihaji Makame akijibu maswali
ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi yaliowasilishwa katika Kikao hicho
kuhusiana na Wafanyabiashara wa Jua Kali na Wanaouza Samaki nje ya Soko
la Marikiti Darajani. (Picha ya pili kulia) Waziri
wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe.Nassor Mazrui akijibu maswali ya
Wajumbe wa Baraza kuhusiana na Wakulima wa Mwani Zanzibar hatma ya bei
ya Zao hilo katika soko la Zanzibar bei yake iko shilingi 300/= na
wengine hununua shilingi 400/=
Mhe. Ali Mzee Ali, Mhe. Mansoor Yussuf Himid na Mhe. Mbarouk Mtando,
wikitoka katika Ukumbi wa Baraza baada ya kuahirishwa kwa ajili ya
matayarisho ya Kikao cha Kuwasilisha Bajeti ya Serekali leo jioni.
Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Jazira, akisisitiza jambo na
Mwakilishi wa Bububu Husein Ibrahim Makungu BHAA,wakiwa nje ya ukumbi
wa mkutano baada ya kuahirishwa leo asubuhi.
Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa akibadilishana mawazo na Wajumbe wa Baraza wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano leo asubuhi.
Comments