MSHAMBULIAJI Amri Kiemba amesema kwa sasa ameamua kufunga mjadala kuhusu
mustakabali wake kisoka baada ya kutia saini mkataba mpya wa kuichezea
Simba kwa miaka miwili.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Kiemba alisema si kweli kwamba alikuwa katika harakati za kurejea katika klabu yake ya zamani ya Yanga.
"Unajua mimi si muongeaji sana. Wakati magazeti yanaandika mimi nimesaini mkataba na Yanga, nilikuwa nashangaa sana, lakini sikutaka kujibu. Sasa ukweli ni huu, nimeingia mkataba na Simba kwa miaka miwili zaidi,"alisema.
Kiemba alisema kwa sasa anaelekeza nguvu zake katika timu ya Taifa, Taifa Stars, ambayo inajiandaa kumenyana na Ivory Coast katika mechi ya michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za 2014.
"Naamini mjadala wa Kiemba umekwisha salama, sasa ni zamu ya wengine,"alisema.
Kiemba alimwaga wino Simba juzi mbele ya Kaimu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang'are, maarufu kwa jina la Mzee Kinesi.
Kiungo huyo alimwaga wino Simba siku moja baada ya kurejea kutoka Morocco, ambako alikwenda kuichezea Taifa Stars katika mechi dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo.
Kiemba alikuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wa Morocco kutokana na kuifungia Taifa Stars bao la kujifariji kwa shuti kali la umbali wa mita zipatazo 25. Katika mechi hiyo, Taifa Stars ilichapwa mabao 2-1.
Baada ya mchezo huo, mashabiki wa soka wa Morocco walianza kumfuatafuata Kiemba wakiomba kupiga naye picha na walimtambua kwa urahisi kutokana na rasta zake.Inatoka kwa mdau.

Comments