Na Bosire Boniface, Garissa
Kenya inajiandaa kusambaza ndege zisizo na marubani aina ya 'drones'
kama sehemu ya operesheni za usalama zilizoongezwa katika mipaka yake na
Somalia na Ethiopia kufuatilia na kukomesha harakati za al-Shabaab na
waingizaji wa silaha za magendo, maofisa usalama waliiambia Sabahi.
Vikosi vya usalama vya Kenya vikifanya misheni ya ukaguzi huko Liboi katika mpaka wa Kenya na Somalia mwezi Oktoba 2011 baada ya wafanyakazi wawili wa msaada wa Kihispania kutekwa katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab. [Tony Karumba/AFP]
Ndege aina ya 'drones', au vyombo vya angani visivyo na marubani,
zinahitajika kusaidia vikosi vya usalama vya Kenya kufanya doria katika
mipaka ya nchi, alisema Patrick Ochieng, mkurugenzi wa Eneo Lengwa La
Kitaifa la Kenya kuhusu Silaha ndogondogo na Silaha Nyepesi.
"Tunakabiliwa na changamoto za ulinzi ambazo hazijawahi kutokea,"
aliiambia Sabahi. "Sio tu kuwa tuna vitisho kutoka ndani ya nchi, bali
pia kutoka kwa waasi wa al-Shabaab."
Uingizaji silaha kwa magendo na upenyezaji unaofanywa na al-Shabaab
katika mkoa wa kaskazini-mashariki wa Kenya umeleta hali ya kutokuwa na
usalama pamoja na athari mbaya, alisema, akiongeza kwamba miaka miwili
iliyopita imeshuhudia ongezeko la vurugu kutokana na bunduki haramu, kwa
wahalifu na wauza silaha kwa magendo kuzua njia mpya za kuuza silaha
kwa magendo.
Polisi wa Kenya wenye hadhi ya kijeshi
jijini Nairobi wakilichoma rundo hili la silaha haramu zilizokamatwa
mwezi Machi 2009. [Simon Maina/AFP]
Ndege zisizo na marubani zitawekewa teknolojia ya kiwango cha juu ikiwa ni pamoja na kamera zinazoweza kuona usiku ili kuisaidia Kenya kuwashinda wahalifu na kuondoa vitisho vya usalama, Ochieng alisema.
Ndege zisizo na marubani zitawekewa teknolojia ya kiwango cha juu ikiwa ni pamoja na kamera zinazoweza kuona usiku ili kuisaidia Kenya kuwashinda wahalifu na kuondoa vitisho vya usalama, Ochieng alisema.
Maofisa usalama wanapata mafunzo kuhusu ndege zisizo na marubani, ambazo
zitaanza kazi mwishoni mwa mwaka huu, alisema Ochieng. Alikataa kupeana
maelezo zaidi kuhusu programu hiyo, alisema kwamba kwa kufanya hivyo
kutasaidia wanaoingiza silaha nchini.
Comments