Mbeya/Dar. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman ameweka bayana kuwa wanaunga
mkono Rasimu ya Katiba na hasa suala la Muungano wa Tanzania kuundwa na
Serikali tatu kama ilivyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman
Amesema mambo mengi yaliyopendekezwa na chama chake yamefanyiwa kazi na
Tume ya Mabadiliko na kuishangaa CCM akidai kwamba inapinga rasimu hiyo
hususan suala la Serikali tatu wakati kimsingi watu wa Tanzania Bara
wamekuwa wakipunjika kwenye muundo wa sasa wa Muungano.
Akihutubia mkutano wa kampeni ya kuwania udiwani wa Kata ya Iyela katika
Uwanja wa Bongonela, Mbeya jana jioni, Mbowe alisema chama chake
kinataka kuona Serikali ya Tanganyika ikifufuliwa. Alikuwa akimnadi
mgombea wa Chadema, Charles Mkela.
Alisema Chadema kinataka kuona Wazanzibari wakiwa na Serikali yao ili
wajiamulie mambo yao na pia Watanganyika wawe na uongozi wao lakini
waunganishwe na Serikali ya Muungano.
Alisema muundo wa sasa wa Muungano una matatizo. Kwa mfano, mbunge wa
Zanzibar anawakilisha watu wachache zaidi ukilinganisha na mbunge wa
Bara. Wananchi mtashangaa sote tunalipwa sawa.”
“Ila zikija Serikali tatu ina maana kuwa kila upande wa Muungano
utatumia rasilimali zake. Haya mambo kulipana fedha nyingi kwa kazi
kidogo yatakoma.”
Comments