Dar/Dodoma. Rasimu ya Katiba Mpya iliyozinduliwa jana, imependekeza
kupunguzwa kwa madaraka ya Rais wa Tanzania maeneo tofauti ya utendaji
wake, ukiwamo uteuzi wa viongozi na watendaji wakuu wa Serikali.
Tume hiyo inapendekeza kwamba Rais ashirikiane na mihimili mingine ya
dola katika uteuzi huo, huku ikiwataja Mawaziri na Naibu Mawaziri, Jaji
Mkuu, Naibu Jaji Mkuu na Katibu Mkuu Kiongozi kuwa uteuzi wao
utakapofanywa na Rais lazima uthibitishwe na Bunge.
Mapendekezo hayo ni tofauti na hali ilivyo sasa wakati uteuzi unaofanywa
na Rais hauthibitishwi na Bunge, isipokuwa nafasi ya Waziri Mkuu na
Makamu wa Rais itapotokea ikawa wazi kwa sababu zozote zile.
Pia, tume inapendekeza Rais ashauriane na chombo kipya kitakachoundwa
cha Baraza la Ulinzi la Taifa kuwateua viongozi wote wa taasisi za
ulinzi nchini.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba alisema
mfumo wa utawala utaendelea kuwa kama ulivyo hivi sasa na kwamba, Rais
ndiye mtendaji wa Jamhuri ya Muungano na atachaguliwa moja kwa moja na
wananchi.
Jaji Warioba alisema Tume imependekeza mgombea urais lazima apate zaidi
ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa na kwamba, kinga ya kutokuhoji
matokeo ya uchaguzi mahakamani iondolewe.
“Mgombea urais anaweza kupendekezwa na chama cha siasa au kuwa mgombea
huru, mgombea wa nafasi hiyo atatangazwa kuwa mshindi iwapo atakuwa
amepata zaidi ya asilimia 50 ya kura zote zilizopigwa,” alisema Jaji
Warioba na kuongeza:
Comments