Dodoma.
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwigulu Nchemba jana nusura wachapane makonde baada ya kutupiana maneno ya kashfa, wakituhumiana kuhusika na mlipuko wa bomu uliotokea Jumamosi iliyopita mkoani Arusha.
Tukio hilo lilitokea katika viwanja
vya Hoteli ya St Gasper nje kidogo ya mji wa Dodoma, walipokwenda kwa
ajili ya kuhudhuria semina ya wabunge wapambanaji na Ukimwi, ambapo
baadhi ya wabunge wa Chadema walihudhuria, baada ya kutoonekana mjini
humo tangu Juni 17 mwaka huu.
Wabunge hao wa Chadema hawakuhudhuria
kikao chochote cha Bunge kutokana na kwenda mkoani Arusha kwa shughuli
mbalimbali, kutokana na mlipuko wa bomu uliotokea katika mkutano wao wa
kuhitimisha kampeni zake za uchaguzi mdogo wa udiwani katika viwanja vya
Soweto, Juni 16 jijini humo.
Malumbano hayo yanatokana na Nchemba
kuituhumu Chadema kuhusika na mlipuko huo, Juni 20 mwaka huu wakati
akichangia hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka 2013/2014, akisema
chama hicho kilipanga kulipua bomu hilo ili kuwafanya Watanzania waamini
kuwa Serikali ya CCM ndiyo inayohusika na tukio hilo.
Ilivyotokea
Wakati Msigwa akiingia katika ukumbi
huo akiwa ameongozana na Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekiah Wenje,
walikutana uso kwa uso na Nchemba ambaye alikuwa akizungumza na Makamu
Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour Arfi.
Baada ya Nchemba kumwona Msigwa alimkaribisha mchungaji huyo akisema; “Karibu sana bwana, salama lakini?”
Hata hivyo, badala ya kujibu salamu
hiyo ya Nchemba, Msigwa alikuja juu na kumtuhumu Nchemba kwamba anatoa
kauli zinazoweza kuvuruga amani ya nchi.
“Wewe ni mtu hatari sana, haya yote
yanasababishwa na wewe, mnatumia damu za watu kutafuta madaraka,”
alisema Msigwa akimtupia maneno Mwigulu.
Baada ya kauli hiyo Nchemba alihoji akisema: “Ki-vipi? Hayo mambo tuyaache, Msigwa achana na haya mambo!”
Baada ya Nchemba ambaye pia ni Naibu
Katibu Mkuu wa CCM kujibu, Msigwa alimsogelea karibu na kumnyooshea
kidole, huku akiendelea kumtuhumu kuwa ana siasa chafu zinazopandikiza
chuki kwa jamii.
Malumbano hayo pia yaliingiliwa na
Mbunge wa Musoma Mjini (Chadema), Vicent Nyerere ambaye alimuunga mkono
Msigwa, huku akimtuhumu Nchemba kuwa ni mtu mbaya katika siasa za
Tanzania. Katika kile kilichoonekana kutaka kuweka mambo sawa, Wenje
alimvuta Msigwa na kumpeleka ukumbini ili kuepusha shari baada ya
wabunge hao kuzidi kurushiana maneno. Soma zaidi...
http://www.mwanachi.co.tz
Comments