Na Othman Khamis Ame
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetuma salamu za rambi mbali kwa Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Muhongo kutokana na vifo vya wananchi
watatu wa Mkoa huo vilivyotokea kufuatia mripuko wa bomu uliotokea juzi
katika viwanja vya Soweto Jijini Arusha.
Watu wasiopungua 70 waliripotiwa kujeruhiwa wakati wa mripuko huo kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Soweto wa
Chama cha Demokrasia ya Maendeleo { Chadema }.
Katika Taarifa ya rambi rambi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
iliyotumwa kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha na kutiwa saini na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea kupokea kwa
masikitiko na huzuni taarifa ya shambulio la kigaidi la bomu lililotokea
tarehe 15 Juni mwaka 2013.
Balozi Seif alisema Taifa kwa mara nyengine tena limekumbwa na msiba wa
njama za kigaidi zilizoua na kujeruhi rMkuu wa Koa wa Arusha aia wema
wasio na hatia sambamba na tukio jengine linalofanana na hilo
lililogharimu roho za wananchi wengine wakati wakiwa katika ibada
Kanisani.
Balozi Seif alisema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Wananchi na yeye binafsi anatuma salamu hizo za rambi rambi kutokana na
maafa hayo na kuwaombea marehemu malazi pema na majeruhi wapone haraka
ili waungane na wenzao katika ujenzi wa Taifa.
Comments