Kushoto ni Rais wa Marekani Barack Obama, kulia ni mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
REUTERS/dailymail
Rais wa Marekani Barack Obama atakutana na familia ya mwasisi wa Taifa
la Afrika Kusini Nelson Mandela, wakati huu ambapo shujaa huyo wa vita
dhidi ya ubaguzi wa rangi akiwa katika mapambano dhidi ya maradhi ya
mapafu yaliyosababisha kuzorotesha afya yake.
Taarifa toka nchini humo zimeeleza kuwa Obama ameamua kutomtembelea
shujaa huyo hospitalini anakopatiwa matibabu mjini Pretoria ili
kudumisha amani na utulivu katika eneo hilo.
Rais wa Marekani Barack Obama, kulia ni mwenyeji wake Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
REUTERS/dailymail
Obama amesema kuwa hakuwa na haja ya muda wa kupiga picha na Mandela
kufuatia uvumi kwamba angeweza kumtembelea hospitalini kinara huyo wa
vita dhidi ya ubaguzi wa rangi na mshindi mwenzie wa tuzo ya amani ya
Nobeli ambaye amelazwa katika hospitalini kwa zaidi ya majuma matatu
sasa.
Obama, ambaye alikutana Mandela mara moja jijini Washington mwaka 2005,
amesema kuwa jambo la msingi kwake ni kumpa faraja Rais huyo wa zamani
wa Afrika Kusini na ustawi wa familia yake.
Rais huyo wa marekani ameyazungumza hayo mjini Pretoria mara baada ya
mazungumzo yake na Rais wa sasa wa Afrika kusini, Jacob Zuma.
Ziara ya Rais Obama nchini Afrika Kusini haijawa na mvuto kama
ilivyotarajiwa kutokana wananchi wa Taifa hilo kuelekeza zaidi macho na
masikio yao katika maendeleo ya afya ya kiongozi wao wa zamani.
Via kiswahili.rfi.fr
Via kiswahili.rfi.fr
Comments