Meya Jerry Silaa awataka Watanzania kutunza na kulinda afya zao ili kujenga familia na jamii yenye afya bora.
Akitoa nasaha wakati wa kufunga wa zoezi la utoaji wa huduma za afya kwa
uwiano katika jamii kata ya Gombo la Mboto, Mgeni rasmi Mh. Jerry
Silaa, Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya Ilala amesema huduma
za afya na afya ya mazingira ni muhimu katika maisha ya kila siku ya
binadamu.
Wananchi wa Tanzania wameelezwa kuwa kazi ya kuboresha huduma za afya na
afya ya mazingira na maji ni ngumu na kuwa inahitaji nguvu za pamoja
kati ya jamii, halimashauri na wadau mbalimbali ili kupata mafanikio
yaliyokusudiwa hasa ya uzuiaji wa magonjwa.
Aidha amesema hilo ni moja wapo katika utekelezaji wa agizo la Mh. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika lengo lake la kupeleka huduma
za tiba zikiwamo zile za zinazohitaji madaktari bingwa karibu na
wananchi.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala Dr. Asha Mahita akielezea dhamira ya
Idara katika kuendeleza Afya ya Jamii kwa kusogeza Huduma za Afya karibu
na Jamii, Huduma hizo zinahusisha matibabu kwa magonjwa mbalimbali kama
Magonjwa ya Moyo, Kisukari, Malaria, Macho, Meno, Afya ya Akili,
Ushauri na kupima VVU kwa hiari, Elimu juu ya Uzazi wa Mpango na Afya ya
Uzazi, Afya ya Mazingira, Lishe, na Jinsia, pia ametoa tathmini ya
wakazi wa Kata ya Gongo la Mboto Markaz waliopatiwa huduma za Afya bure
kwa zoezi lililofanyika kwa muda wa siku tatu ikiwemo Afya ya Akili,
Kifua Kikuu na matibabu ya Ujumla.
Kwa tasira zaidi tembelea MOBLOG
Comments