Na Majid Ahmed, Mogadishu
Wakaazi, wazee wa kimila na maofisa wa serikali nchini Somalia kote
wanatoa wito kwa wanamgambo wenye uadui wa kurithi juu ya udhibiti wa
Kismayo kuweka silaha chini na kuja katika meza ya mazunguzmo kutatua
masuala yaliyobakia na kuhakikisha maisha ya amani yanarejea.
Wanachama wa Jeshi la Taifa la Somalia na
wanamgambo wa Ras Kamboni walioshirika na serikali wakipeperusha bendera
ya Somalia kutoka kwenye uliokuwa mnara wa kuongozea ndege katika
uwanja wa ndege wa Kismayo katika kushereheka kukamatwa kwake tarehe 2
Oktoba, 2012. [AFP Photo/AU-UN IST Photo/Stuart Price]
Vurugu zilizokuwa zimesimama zilianza tena Ijumaa (tarehe 7 Juni) baada
ya wanamgambo wa Ras Kamboni wanaomtii Shekhe Ahmed Mohamed Islam Madobe
kuripotiwa kuweka wazi kuwa kiongozi wa wanamgambo hao Iftin Hassan
Basto kutoka kwenye mkutano na Waziri wa Ulinzi wa Somalia Abdihakim
Haji Mohamud Fiqi. Madobe, Basto na Barre Adam Shire Hirale wote kwa
sasa wamelaumiwa kwa kuwa watiifu kwa raisi aliyeteuliwa wa serikali
changa ya shirikisho ya Jubbaland.
Mapigano makali yaliibuka, yaliua watu wapatao 18, yakijeruhi wengine
zaidi ya 20 na kulazimisha mamia ya wakaazi kukimbia na kutafuta hifadhi
katika vijiji vya jirani, kwa mujibu wa Nur Abdirahman, mkaazi mwenye
umri wa miaka 38.
Familia ya watu watano mtaani wake walikuwa miongoni mwa waathirika,
Abdirahman alisema, wakati magamba ya mota yalipodondoka katika nyumba
yao ya wastani .
"Tunachotaka tu ni hali kuimarika," aliiambia Sabahi. "Tunamwomba Mungu
kwamba mapigano haya yamalizike kabisa na kamwe tusikie tena milio ya
mota au risasi huko Kismayo."
Comments