MWANADADA Mahiri katika uigizaji wa filamu Swahiliwood Riyama Ali
amewashukia baadhi ya wasanii ambao ujisahau baada ya kutoka katika
uigizaji wa filamu na kuwa nyota, Riyama anasema kuwa amewasaidia
wasanii wengi kisanaa lakini badala yake wamegeuka maadui wala hawana
hata shukrani kwake tabia hiyo anaamini ipo sana kwa wasanii wengi
wachanga wakitoka.
.
.
“Wasanii wa kike tuna tabia ya kujisahau sana katika uhusiano na ni
watu wasiopenda kujulikana walikotoka, unamkutana msichana hana mbele
wala nyuma, anakuja anakufuata kwa maneno matamu ooh dada nakupenda
unavyoigiza natamani niwe kama wewe unaonyesha upendo na kumsaidia
akicheza filamu moja tu anaanza kukunanga,”anasema Riyama.
.
.
Aidha mwanadada huyo mwenye uigizaji wa kipekee katika filamu ameenda
mbali baada ya kuwashutumu waigizaji wa kike kwa kukosa kabisa upendo
wa kweli na kuwa waigizaji hata katika maisha ya kawaida jambo ambalo
linawafanya wadharauliwe katika jamii yao, hadi imefikia kwa msanii
anayejielewa kuchukia kuitwa jina la Bongo movie.Inatoka kwa mau.
Comments