Pichani
juu ni maandalizi ya ndani ya Uwanja wa Jamhuri atakapoagwa msanii
Albert Mangweha leo kabla ya mazishi yatakayofanyika nyumbani kwao
Kihonda.
KUFUATIA umati wa watu
uliojitokeza jana kuupokea mwili wa msanii Albert Mangweha, wanafamilia,
ndugu, jamaa na uongozi wa serikali ya mkoa wa Morogoro kwa pamoja
wameamua shughuli za kuaga mwili wa msanii huyo zifanyike ndani ya
Uwanja wa Jamhuri badala ya nyumbani kwao marehemu eneo la Kihonda
Mazimbu Road kama ilivyokuwa imetaarifiwa hapo mwanzo.
Comments