Ligi Kuu ya Bara inatarajiwa
kuendelea wikiendi hii kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja mbalimbali
nchini, huku kila timu ikisaka ushindi katika michezo hiyo ili kujiweka katika
mazingira mazuri kwenye msimamo wa ligi.
Jumamosi, Young Africans watakua
wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku
Ndanda FC wakiwakaribisha wakata miwa wa Kagera Sugar katika uwanja wa
Nang’wanda Sijaona mjini Mtwara.
Coastal Union watawakaribisha
maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Mkwakwani jinini Tanga, huku Jumapili,
Simba SC wakicheza dhidi ya Toto Africans katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam
Comments