Mchezaji wa zamani wa Ligi Kuu Fernando Torres aliifungia goli la
kuongoza Atletico Madrid katika dakika ya 25 katika Uwanja wa Nou Camp.
Nyota huyo wa Atletico Madrid alionyeshwa kadi nyekundu dakika 10 baadae baada ya kumchezea vibaya Sergio Busquets.
Luis Suarez alisawazisha goli la Torres katika kipindi cha pili katika mpambano mkali wa robo fainali Ligi ya Mabingwa.
Mchezaji huyo wa Uruguay alifunga goli la pili la ushindi baada ya kupiga kichwa kilichomzidi mlinda mlango Jan Oblak.
Nao Bayern Munich walishinda goli moja dhidi ya Benfica ya Ureno, goli likifungwa na Arturo Vidal.
Comments