Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF), Issa
Hayatou amemtumia salamu za pongezi Ravia Idarous Faina kwa kuchaguliwa
kuwa Rais wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) mwishoni mwa juma
lililomalizika.
Katika salamu zake, Hayatou amesema kwa niaba ya CAF, Kamati ya
Utendaji na yeye binafsi wanampongeza kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama
cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA).
CAF wanaimani na uzoefu wa Ravia katika uongozi, kuwa ataendeleza uongozi bora kwa faida ya maendeleo ya soka visiwani Zanzibar.
Aidha Hayatou amewatumia pia salamu za pongezi, Mzee Zam Ali na Ali Mohamed kwa kuchgauliwa kuwa makamu wapya wa Rais wa ZFA.
Hayatou amewatakia mafanikio mema katika nafasi mpya hizo
walizochaguliwa na kuahidi CAF itaendelea kuwapa ushirikiano wa
maendeleo ya mpira wa miguu visiwani Zanzibar.
Comments